Verse 1
Umoja ni fahari yetu
Undugu ndio nguvu
Chuki na ukabila
Hatutaki hata kamwe
Lazima tuungane, tuijenge nchi yetu
Pasiwe hata mmoja
Anaetenganisha
Chorus
Naishi, Natumaini,
Najitolea daima Kenya,
Hakika ya bendera
Ni uthabiti wangu
Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
Daima mimi mkenya
Mwananchi mzalendo
Verse 2
Kwa uchungu na mateso
Kwa vilio na uzuni
Tulinyakuliwa Uhuru
na mashujaa wa zamani
Hawakushtushwa na risasi
au kufungwa gerezani
Nia yao ukombizi kuvunja pingu za ukoloni
Chorus
Naishi, Natumaini,
Najitolea daima Kenya,
Hakika ya bendera
Ni uthabiti wangu
Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
Daima mimi mkenya
Mwananchi mzalendo
Verse 3
Wajibu wetu
Ni Kuishi kwa upendo
Kutoka ziwa Mpaka pwani
Kaskazini na kusini
Chorus
Naishi, Natumaini,
Najitolea daima Kenya,
Hakika ya bendera
Ni uthabiti wangu
Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
Daima mimi mkenya
Mwananchi mzalendo